×

Mamadou Sakho Balozi wa Utalii Tanzania

Mchezaji wa Crystal Palace ya Uingereza na timu ya taifa ya Ufaransa Mamadou Sakho, akubali kuwa balozi wa Utalii Tanzania.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii @tanzania_unforgettable (TTB) Betrita Lyimo akiwa pamoja na Mamadou Sakho @mamadousakho , Mchezaji wa mpira wa miguu kilabu ya Crystal Palace @cpfc inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na mchezaji wa timu ya Taifa ya Ufaransa.

Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu wa Kilabu ya Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL) na Mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa amekubali ombi la Bodi ya Utalii Tanzania @tanzania_unforgettable (TTB) kuwa Balozi wa Hiyari wa Utalii wa Tanzania.

Mamadou amekubali ombi hili wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.

 

Mamadou ambaye ni raia wa Ufaransa amewasili nchini Tanzania tarehe 26/5/2021 kwa mapumziko ya siku 10 akiwa ameambatana na familia yake wametembelea vivutio vya utalii vya Hifadhi ya Taifa ya @serengeti_national_park, Kijiji cha Wamasai cha Seneto, Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro na Visiwa vya Zanzibar.

Leave a Comment