Nahodha wa timu ya Taifa, ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa Klabu ya Fenerbahce ya Ligi Kuu ya Uturuki, Mbwana Samatta leo Juni 1, 2021 ametembelea Kiwanda cha Cocacola kujionea hatua za utengenezaji wa kinywaji hicho. Samatta ambaye pia ni mwakilishi wa Coca-Cola Tanzania wa kuitangaza chapa ya kampuni hiyo katika kampeni zake ili kuwahamasisha Watanzania kufikia ndoto zao, alishirika kwenye uzinduzi wa kampeni ya ‘WASHA MDUNDO.’