×

Apple Music Yafanya Jambo, Tiwa Savage Atia Neno

AFRICA Now Radio inayopatikana kwenye platform ya Apple Music 1, imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.

 

Zaidi ya vipindi 52 vilivyorushwa kupitia redio hiyo vikiongozwa na mtangazaji Cuppy, yakiwemo mahojiano na wasanii wakubwa barani Afrika, vimefanya redio hiyo kuwa maarufu, ikiangazia bara lote la Afrika na kuonesha mwanga kwa mastaa wa vizazi vijavyo.

 

Katika maadhimisho hayo,  mtangazaji Cuppy anatupitisha katika kipindi maalum cha kuangazia matukio muhimu, yakiwemo mahojiano na wasanii wakubwa na wasanii waliobamba chati mbalimbali za Afrika kwa kipindi cha miezi 12, akichanganya na ladha zake zilizoifanya redio hiyo kuwa tishio.

BAADHI YA MAHOJIANO

Cuppy anaeleza kwamba katika intavyuu zote alizozifanya, ile ya Tiwa Savage aliyoifanya katika Kipindi cha Staa wa Wiki, Episode 7 ni miongoni mwa intavyuu bora kabisa kwake.

 

Katika mahojiano hayo, Tiwa Savage analezea jinsi anavyoishi maisha yake ya kistaa na kumfanya kuwa miongoni mwa mastaa wanaotrend, pamoja na ngoma alizoziachia katika albamu (EP) yake ya Celia.

https://music.apple.com/us/curator/africa-now-radio-with-lootlove/1494794631

Katika mahojiano ya Kipindi cha Staa wa Wiki anawataja wasanii anaowapenda, aliowashirikisha katika albamu yake ya For Broken Ears kwenye Episode ya 19; huku Davido akifurahia kuitwa baba na kuelezea mambo mengi kuhusu muziki wake, kwenye Episode ya 25.

NYIMBO BORA

Kuhusu nyimbo bora zilizotamba mwaka mzima, Cuppy anazitaja ngoma kali kutoka kwa wasanii Burna Boy, Tiwa Savage, Rema, Cassper Nyovest feat. Lady Du, Ayra Starr, Tems, Davido feat. CKay, Otile Brown & Kizz Daniel, Sha Sha na Kuami Eugene.

 MINI MIX

Katika kufunga shoo ya wiki, Cuppy anashusha mixing kali ya nyimbo zake anazozipenda, zilizotamba kwa kipindi cha miezi kumi na mbili iliyopita, zote zikiwa zimetamba kwenye jukwaa la Apple Music’s Africa Nowplaylist.

 

Katika mixing ya wiki hii, kuna nyimbo kutoka kwa KiDi, Nelson Freitas, KDDO, Yemi Alade, Master KG, Sho Madjozi na wengine wengi.

Leave a Comment