
Wakati huko kwenu mtoto mwenye umri wa miaka saba anacheza cha ndimu na kibaba na mama, hali ni tofauti kwa Kapteni Graham Shema kutoka uganda.
Graham ana umri wa miaka saba tu, lakini ni fahari ya Uganda kwa sababu anapendwa na vyombo vya habari na pia watu wa Taifa lake.
Kufuatia safari yake ya kwanza ya ndege akiwa rubani mdogo zaidi, amekua gumzo nchini mwake.
Watu katika nchi yake, ambao wamevutiwa na uwezo wake kama rubani mchanga, wamempa jina la ‘Nahodha’ kwa sababu yeye ni rubani aliyefanikiwa sana akiwa mdogo zaidi.
Awali, Graham alirusha ndege tatu za injini moja za viti vinne zinazojulikana kama 172 Cessna wakati bado ni rubani wa mafunzo.
Baadaye ndipo akaweza kurusha ndege kadhaa jambo iliyosababisha watu wengi kumtambua na kujulikana kote ulimwenguni.
Graham mwenye vipaji vingi ana shauku kubwa kuwa rubani wa ndege kwa muda mrefu na anatarajia kuwa mwanaanga na kusafiri kwenda Sayari ya Mars katika siku zijazo.
View this post on Instagram