×

Hukumu ya Mdude wa Chadema Yaahirishwa

MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeahirisha kusoma hukumu ya kesi inayomkabili kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyangali iliyokuwa itolewe leo.

 

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer amesema ameiahirisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake na kubainisha kuwa hukumu hiyo itasomwa Juni 28, 2021.

 

Akizungumza nje ya mahakama, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyehudhuria mahakamani kusikiliza hukumu hiyo, amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu mpaka tarehe iliyopangwa.

 

Mdude anakabiliwa na shtaka la kusafirisha madawa ya kulevya aina ya heroin gramu 23.4, kosa alilolifanya mwaka 2020.

 

Leave a Comment