The House of Favourite Newspapers

Musukuma Ashauri Faini za Bodaboda Ziwe 2000

0

MBUNGE wa Geita Vijijini ,Joseph Kasheku Musukuma, amempongeza Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba, kwa kupunguza tozo kwa madereva bodaboda katika bajeti yake aliyoisoma na kueleza kuwa sula hilo ni miongoni mwa vitu ambavyo Mungu atazidi kumkumbuka na kumuongezea siku za uhai wake

 

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 14, 2021, Bungeni Dodoma, wakati akitoa mchango wake katika Bajeti Kuu ya serikali ya mwaka 2021/2021, iliyosomwa Bungeni Juni 11, 2021, na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba.

 

“Mh. Waziri nakupongeza sana kwenye faini ya bodaboda, nataka nikuambie katika kitu ambacho Mungu atakukumbuka kukuongezea hata siku zako za uhai wako ni suala la faini ya bodaboda, unajua mimi nilikuwa najiuliza wachumi wetu mko namna gani, mimi nilikuwa najiuliza inawezekanaje faini ya bodaboda anayebeba watu wawili unamlinganisha faini na basi la watu 65?, mimi nilikuwa nashauri hata hiyo 10,000 bado ni nyingi tungeweka hata 2000,” amesema Mbunge Musukuma.

 

Leave A Reply