×

Zambia Yatangaza Siku 21 za Maombolezo ya Kaunda

SERIKALI ya Zambia imetangaza siku 21 za maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha muasisi wa taifa hilo Kenneth Kaunda hapo jana, Kaunda anakumbukwa kama baba wa taifa na mkombozi wa Zambia.

 

Bendera zitapepea nusu mlingoti na matukio yote ya burudani yamepigwa marufuku kwa heshima ya kiongozi huyo wa zamani aliyekuwa na haiba kubwa.

 

Rais wa sasa wa Zambia Edgar Lungu alisema Kaunda amefariki wakati ambao hawakutarajia, huku akimueleza kuwa kiongozi halisi wa Afrika.

Katibu wa baraza la waziri Simon Miti alisema katika hotuba kwa umma wa Zambia kupitia runinga kwamba Kaunda alikufa kwa amani mida ya nane unusu jana katika hospitali hiyo ya jeshi ambako alikuwa akitibiwa tangia Jumatatu.

 

Akifahamika sana kama KK, Keneth Kaunda alikuwa kiongozi wa chama kilichoiongoza Zambia baada ya uhuru kutoka kwa utawala wa kikoloni wa Uingereza.

 

Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, aliandika katika ukurasa wake wa twita akisema amehuzunishwa na taarifa za kifo cha Kaunda na kutuma risala za rambirambi kwa watu wa Zambia.

 

Leave a Comment