The House of Favourite Newspapers

Simba Yanusa Ubigwa Ikiichapa Mbeya City 4-1

0

ZIMEBAKI alama tatu ndivyo walivyotoka uwanjani mashabiki wa Simba jana Juni 22. kwenye uwanja wa Mkapa baada ya kuipiga Mbeya City magoli 4-1, kwenye mchezo wa ligi kuu bara uliocheza jana usiku

 

Simba ambao waliingia na mfumo wa 3-5-2 walifanikiwa kuapachika magoli mawili kwenye kipindi cha kwanza kupitia kwa Larry Bwalya, dakika 31, na Luis Miquissone dakika ya 35.

Kipindi cha pili nahodha John Bocco aliandikia Simba goli la tatu ikiwa ni goli la 14 msimu huu kwenye Vpl, baada ya goli hilo Mbeya City  walionekana kucharuka na kufanikiwa kufunga bao dakika ya 51 kupitia kwa Pastory Athanas.

 

Wekundu wa Msimbazi walihitimisha karamu hiyo kupitia kwa mwamba wa Lusaka Claotus Chama dakika ya 86 baada ya kumalizia pasi safi kutika kwa beki wa beki wa kulia Shomari Kapombe.

 

Kwa jinsi hali iliyo ni dhahiri Simba inahitaji alama tatu ili itawazwe kuwa mabingwa kwa msimu huu 2020/21 kwa sasa wanaongoza ligi hiyo wakiwa na alama 73, baada ya kucheza michezo 29, Yanga nafasi ya pili na alama 67 wakicheza michezo 31.

 

Leave A Reply