
Rais Samia Suluhu Hassan leo Juni 29, 2021 amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Afrika wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Abebe Aemro Selassie, Ikulu jijini Dodoma na kufanya naye mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo jinsi shirika hilo litakavyoisaidia Tanzania katika kukabiliana na ugonjwa wa Corona.
Abebe amesema IMF ipo tayari kuendelea kufanya kazi na wataalamu wa Tanzania kuandaa andiko litakalowezesha kupata msaada wa fedha kwa ajili ya kupambana na athari zitokanazo na ugonjwa wa Corona.
Ameongeza kuwa IMF itaisaidia Tanzania kupata fedha kwa ajili ya kuimarisha sekta zilizoathirika na Corona ikiwemo sekta ya utalii, maji na afya.

