×

Rais Samia Mgeni Rasmi Maonesho Ya 45 Ya Sabasaba

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Kitila Mkumbo (Mb) amekagua maandalizi ya maonesho ya 45 ya Sabasaba yaliyoanza rasmi tarehe 28 Juni, 2021 na kuridhika na hatua nzuri za ukamilishaji wa baadhi ya mabanda.


Mkumbo ameyazungumza hayo tarehe 28 Juni, 2021 alipotembelea maonesho hayo ya 45 ya Sabasaba ambayo yatazinduliwa rasmi tarehe 5 Julai, 2021 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.


Prof. Mkumbo amezungumza na waandishi wa habari kuhusiana na jinsi Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilivyojipanga kuhakikisha maonesho haya ya mwaka huu yenye kauli mbiu ya “Uchumi wa Viwanda kwa Ajira na Biashara Endelevu” yanakuwa mazuri na ya mfano.


Mhe. Prof. Mkumbo amesema kuwa mwaka huu kutakuwa na washiriki 3,002, taasisi za umma na binafsi zitashiriki na pia kumekuwa na ongezeko la nchi zitakazoshiriki mwaka huu kutoka nchi tano hadi nchi saba ambapo makampuni ya kigeni ni sabini na sita 76.


Mhe. Prof. Mkumbo ameeleza kuwa mwaka huu kutakuwa na mikutano ya mitandao ya B2B itakayowakutanisha wafanyabiashara wa nje na wa kwetu katika kutafuta fursa za uwekezaji.


Pia kutakuwa na nembo maalumu ya banda maalumu ya viungo vya vyakula vinavyozalishwa nchini na uzinduzi huo utafanyika tarehe 9 Julai, 2021, pia uzinduzi wa mfumo rasmi wa taarifa za biashara, pia kutakuwa na uzinduzi wa duka la mtandao unaoanzishwa na Tantrade kwa kushirikiana na benki ya posta, pia kutakuwa na uzinduzi wa Trailer lililotengenezwa na Kilimanjaro Machine Tools, uzinduzi wa utambuzi wa mabanda ya washiriki wa ndani ya uwanja.
Mhe. Mkumbo amewataka wanachi kujitokeza kwa wingi kwani viingilio ni nafuu kwa kila Mtanzania kuja kujionea biashara mbalimbali na kupata fursa mbalimbali.

LIVE: MAGAZETI JUNE 30: KAULI YA SAMIA YAZUA MJADALA ATOA MWELEKEO

Leave a Comment