×

DC Jokate Azindua Mabanda Ya Wasanii Sabasaba

Viwanja vya Sabasaba leo Julai 1, 2021 kumefanyika uzinduzi wa mabanda ya maonesho ya biashara za wasanii yaliyopewa jina la ‘Meet Your Star’ ambapo Mgeni rasmi ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Jokate Mwegelo.

Maonesho ya mabanda ya wasanii yalianzishwa na Mtangazaji Zamaradi Mketema mwaka 2020 na mwaka huu yanafanyika kwa mara ya pili ambapo Mastaa ambao tayari wameshaweka mabanda yao ni pamoja na Shilole, Zamaradi, Kajala, Flaviana Matata na wengine.

Mabanda hayo yaliobuniwa na mtangazaji na mmiliki wa Zamaradi Tv, Zamaradi Mketema.

  

Leave a Comment