×

Mbunge wa CCM Singida Atoa Bima za Afya Kwa Wanawake 400

MBUNGE wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Singida, Martha Gwau ametoa bima za afya kwa wanawake 400 mkoani hapa ili ziwasaidie kupata matibabu.MGwau alitoa bima hizo jana wakati
akihutubia kwenye kongamano la wanawake Mkoa wa Singida lililofanyika Ukumbi wa Chuo cha Utumishi wa Umma ambapo pamoja na mambo mengine walitafakari siku 100 za Rais Samia Suluhu Hassan za kuwa madarakani na mafanikio ya wanawake hapa nchini huku kauli mbiu ikiwa ni ‘Wanawake ni Nguzo ya Maendeleo’ Kazi
iendelee.

” Bima hizi  ni  zawadi ya Afya kutoka katika mfuko wa ofisi yangu na nijuhudi za kumuunga mkono Rais wetu
Samia Suluhu Hassan katika kuboresha afya za akina mama kwani bila afya hakuna  maendeleo na ili maendeleo yaje na kufanya kazi kwa bidii ni budi kila mtu kuwa na afya njema, hivyo nimeamua kugharamia suala la afya kupitia mfuko wa bima wa CHF kwa wanawake hawa ambao ni sawa na kaya 400 huku wanufaika wakiwa 2400
pamoja na watu wenye uhitaji maalumu“.alisema Gwau.

Alisema bima hiyo itakuwa  ya watu sita kutoka kwenye kila familia ya wanawake hao 400.

Gwau alisema mwaka huu ameanza na kaya 400 lakini matarajio yake ni kufikisha kaya 1000 na wanufaika wakiwa zaidi ya 5000 itakuwa vizuri zaidi na anafanya hivyo kuunga juhudi za Rais Samia Suluhu
Hassan za kuwatumikia watanzania katika sekta ya afya.

Pia Gwau alisema kuanzia kesho atatoa utaratibu kwenda kwenye halmashauri zao ambako anatoka kila mwanamke kwa ajili ya kujisajili ambapo wanatakiwa watu sita yaani baba, mama na watoto wanne walio chini ya umri wa miaka 18.

Gwau alitumia kongamano hilo kwa ajili ya kuwashukuru wanawake hao kwa kumchagua kwa kura nyingi na kuwaomba ushirikiano ambapo pia alieleza mipango na mwelekeo wake wa kazi za maendeleo
mkoani Singida.

Leave a Comment