
Ushawahi kusikia kuwa mapacha wana nguvu kubwa sana za kiroho? Ingawa Wanasayansi bado hawajasema kitu kuhusu hilo, kuna watu wanaosema ni kweli mapacha wana roho flani inayowaunganisha, ila kuna wanaosema ni porojo tu hakuna lolote.
Siku moja mwaka wa 2018 kisa kimoja kilitokea huko India ndicho kilichoaminisha watu kuwa mapacha wana roho moja walioumbiwa na Mungu inayowaunganisha.

Ana Ujauzito Wa Mapacha
Huko India mwaka wa 2018 palitokea mama mmoja kwa jina Hashura aliyekuwa mja mzito. Alipoenda kliniki (clinic) nesi alimwambia kuwa amebeba mapacha tumboni. Ilimpa furaha sana kubarikiwa na mapacha japokuwa hajajifungua bado.
Alikuwa akienda kliniki kama alivyoelekezwa na daktari, huku amefuatana na mume wake. Walipendana sana na mume wake; alimpa ushirikiano kuhusu maisha yote kwa ujumla pale nyumbani. Alimpikia, alimfulia, alimuogesha na kipindi chote cha uja uzito wake alimsaidia kazi zote za ndani. Wana watoto wengine watatu pale nyumbani.

Ajifungua Mapacha Wa Miezi Saba Kwa Njia Ya Upasuaji Kuokoa Maisha
Kama ilivyo kawaida, mwanamke hujifungua akiwa na miezi tisa lakini kwa Hashura ilikuwa ni tofauti kidogo. Hashura akiwa na miezi saba kwenye uja uzito, alianza kusokotwa na tumbo. Bwanake Armaan alimpakiza kwa gari lao na kumuwaisha hospitali kwa ajili ya matibabu.

Hakuwa na mawazo ya kuwa angeenda kujifungua kwani mimba ilikuwa bado changa, bado miezi miwili itimie miezi tisa ya kujifungua. Kama jina lake lilivyo na maana ya uchu, aalikuwa na uchu wa kuwa na watoto mapacha.
Kufika hospitalini, manesi walimwambia Armaan kuwa ilihitajika Hashura kufanyiwa upasuaji ili watoto kutolewa tumboni kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na mapacha wale tumboni. Mungu ni mwema, watoto walitolewa tumboni salama na mama akabaki hai lakini alikuwa hoi.
Armaan alihuzunika huku anamshukuru Mungu kwa kukamilika kwa zoezi hilo la upasuaji. Mapacha walikuwa na kilo moja na kilo moja na nusu mtawalia. Ni ajabu kubwa sana, sio kawaida.

Mama Hoi, Mapacha Hoi, Wote Wanapumulia Mashine Wapo Mahututi
Kwa bahati mbaya, mama na mapacha wake wote walikuwa hoi wanapumulia mashine za Oxijeni. Hali ilikiwa sio hali pale hospitalini kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.
Huzuni ulitanda, Armaan habanduki kwenye chumba cha wagonjwa hao ata sekunde. Hali wala kunywa chochote🥲. Baada ya wiki moja, mama alipata afueni, akapata nguvu ya kupumua mwenyewe bila msaada wa mashine za Oxijeni.

Mama Apata Nguvu Za Kuongea, Awapa Jina Mapacha Wake
Ingawa bado mapacha wapo mahututi, mama aliwapa jina mapacha wake wa kiume na kike Aja na Ajay. Baba yao alibaki anaduwaa tu hajui afanye lipi aache lipi. Aliomba ruhusa kazini akapewa likizo kwa ajili ya kuhudumia familia yake nzima iliyolazwa hospitalini.
Naam, hakuna jambo lisilokuwa na mwisho.
Mwezi mmoja baadaye, kitoto kimoja chenye jina Ajay kilitolewa kwenye mashine baada ya kupata afueni. Acha Mungu aitwe Mungu.
Kilianza kutabasamu, kugeuza shingo lakni Ajay alibakia tu kwenye msaada wa mashine kwenye ‘ Incubator’ hadi akomae, kulingana na maelekezo ya daktari.

Daktari Wawaambia Wazazi Wakiage Kitoto Chao Kwani Hakiwezi Kupona
Wiki mbili baada ya Ajay kuondolewa kwenye mashine, madaktari waliwasikitisha sana wazazi wale kwa kuwaambia kuwa Ajay hawezi kupona kamwe. Waliumia sana, walilia sana. Uchu na furaha ya Armaan kuwa na mapacha ilianza kuzama kwenye bahari ya majonzi.
” Jamani njooni mkiage kitoto chenu, hakiwezi kupona tena. Kinategemea mashine kwa asilimia mia (100%), ” alisema daktari mkuu.
Ona Sasa Miujiza Ya Nguvu Za Roho Za Mapacha
Walijikokota hadi kilipolazwa kile kitoto kichanga kwenye mashine. Daktari akawashauri wamlaze pia Aja pembeni mwake ili amuage mwenzake kabla hajafariki. 💔💔😭😭. Mama alikilaza pembeni na daktari akamuunganisha na mashine pia ya kupumua kama mwenzake.

Kwa kuwa kile kilichowahi kupona kilikuwa na nguvu ya kushika na kugeuka japokuwa fahamu bado ilikuwa haijawa, kilimshika mwenzake mashavuni, mara masikioni na usoni. Huwezi amini, baada ya masaa matatu, Ajay alianza kugezu shingo.
Muda huo huo, anategemea mashine kwa asilimia 50 (50%) na sio asilimia 100 (100%) tena. ” Kwa sasa kuna matumaini kwa sababu sasa hivi Kitoto chenu kinategema mashine kwa 50%. Ni afueni kubwa sana. Ni nguvu iliyoje kwenye roho za mapacha! ” daktari mkuu aliwapa taarifa wazazi.
Ikumbukwe ni siku 51 sasa tangu mapacha wale watolewe tumboni mwa mama zao. Wapo wamekondeana kwa mawazo makubwa sana kuhusu hali ya mapacha wao wa kipekee.

Nguvu Katika Roho Za Mapacha
Daktari walisema kuwa kuna mambo bado wanasayansi hawajakamilisha utafiti wao kuhusu mapacha. Madaktari pale hospitalini na wote walioshuhudia waliafikiana kuwa kuna nguvu kubwa inayowaunganisha mapacha. Aidha, mapacha siku zote wanatakiwa kuishi pamoja. Hatimaye waliruhusiwa kwenda nyumbani kwani mapacha wote walishapona tayari.

Vyombo Vya Habari Vyaripoti Miujiza Hiyo
Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuhusu tukio hilo la kushangaza dunia. Kila mtu alibaki mdomo wazi. Magazeti yalichapisha habari hiyo na picha za mapacha hao zilisambaa kila pembe kwenye mitandao ya kijamii. Familia hiyo ilipokea wageni wenye zawadi kila siku asubuhi, mchana na jioni.
Faraja kubwa sana ilirudi kwa wazazi na walianza kunenepa kwani waliridhika mno.
Oktoba 5, 2019 wazazi wao waliandaa sikukuu ya kuzaliwa kwa mapacha hao, sherehe iliyohudhuriwa na maelfu ya watu. Hakika, walizidishiwa zawadi kibao kutoka kwa watu matajiri nchini waliofika mle kwa magari yao ya kifahari.
Somo la Leo
Usikate tamaa katika maisha, na pia kutokana na hii hadithi ni dhahiri kuwa kuna nguvu za kiroho zinazowaunganisha mapacha. Wanapaswa kuishi pamoja siku zote kwa upendo na mshikamano.