Mke wa aliyekuwa Rais wa Haiti Jovenel Moïse (aliyeuawa jana kwa shambulio), Bi. Martine Moïse (47) hajafariki kama ilivyoripotiwa awali kuwa na yeye amefariki Dunia jioni ya jana Julai 7, 2021 kufuatia majeraha mengi na makubwa aliyoyapata kutokana na shambulio walilofanyiwa yeye na mumewe katika makazi yao, mjini Port-au-Prince.
Bi. Martine amepelekwa Miami Florida nchini Marekani na alishushwa katika Uwanja wa Ndege wa Fort Lauderdale Executive Airport jana mchana na kupelekwa Jackson Memorial Hospital ya kwa ajili ya matibabu zaidi.
