The House of Favourite Newspapers

Okwi Atoweka

0

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Simba ambaye kwa sasa ni mali ya Klabu ya Al Ittohad FC ya nchini Misri, Emmanuel Okwi hajulikani alipo.

 

Kocha wa Al Ittohad FC, Mohammed Mouselhy amesema hawafahamu alipo mshambuliaji huyo ambaye ni raia wa nchini Uganda Mouselhy amesema Okwi ametoweka klabuni hapo bila kutoa taarifa na kitendo hicho wanakichukulia kama utoro.

 

Kocha huyo amesema tayari wamuandikia barua ya kumpa onyo huku taarifa kutoka Uganda zikisema kuwa, Okwi amemaliza mkataba na klabu hiyo tangu Juni 30, mwaka huu.

 

Okwi alijiunga na klabu hiyo mwaka 2019 akitokea kwa mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba SC, lakini amekuwa na wakati mgumu wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza kwenye klabu hiyo.

 

Hivi karibuni, mshambuliaji huyo mwenye kismati na Ligi Kuu Tanzania Bara, alihusishwa na mpango wa kurejea Msimbazi yalipo makao makuu ya Klabu ya Simba SC.

 

Leave A Reply