
Baadhi ya Wahitimu wa Kidato cha Sita mwaka huu waliopata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya Digital Marketing yanayotolewa na mpango wa Airtel Fursa Lab na DTBI wameelezea kunufaika kwao na mafunzo hayo. Wahitimu hao wamesema hayo katika hitimisho la mafunzo hayo yaliyokuwa yakifanyika katika Lab ya Aitel Fursa iliyopo Shule ya Sekondari ya Kijitonyama, Dar.

Akizungumza baada ya kupokea cheti cha kuhitimu mafunzo hayo, Gladness David ambaye ni mhitimu wa kidato cha sita mwaka huu amesema anashukuru kwa kupata mafunzo hayo digital marketing ambayo yamempa mwangaza mkubwa sana katika maisha yake.

“Nashukuru nimejifunza project mbalimbali kupitia digitali marketing ambazo sikuwa nikifahamu kama kupitia mtandaoni unaweza kukutana na fursa mbalimbali za kuweza kujiingizia kipato na kuboresha maisha.

“Kufuatia mambo mbalimbali niliyojifunza kwenye kozi hii sasa naweza hata kujiajiri kupitia fursa nyingi zilizojaa mitandaoni” alimaliza kusema Gladness.
Naye Edson Kizengwa ambaye ni mhitimu wa Sekondari ya Kwiro iliyopo mkoani Morogoro amesema akiwa kwenye fursa hiyo amefundishwa kozi kozi mbalimbali za kompyuta ikiwemo Microsoft, Excel na kudizaini vitu mbalimbali ikiwemo matangazo ya kwenye mabango, majarida na mambo mbalimbali.

Edson amesema kupitia mafunzo hayo sasa ameweza kuijua vizuri kompyuta na kutumia mafunzo aliyoyapata kuweza kujiajiri na kujiingizia kipati chake mwenyewe.
Akizungumza kwenye mahafali hayo Meneja Mradi wa Aitel Fursa Lab, Injinia Michael Thomas amesema walikuwa na mafunzo maalum kwa ajili ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu.
“Mafunzo haya yalilenga kwenye mambo matatu ambayo ni ICT, ubunifu na ujasiriamali.

“Katika mafunzo hayo kwanza tuliwapa mafunzo ya awali ya kutumia kompyuta kiufasaha na kuweza kutatua changamoto mbalimbali katika jamii kupitia teknolojia ya habari na mawasiliano yaani ICT.
“Baada ya kuhitimu wanafunzi hawa tunatarajia kuendelea tena na watu wengine ambapo sasa mtu yeyote anaweza kuja kujifunza ikiwemo wafanyakazi wa maofisini, wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali na wanakaribishwa.

“Mafunzo yanatarajia kuanza wiki ijayo na anayetaka kujiunga kituo chetu kipo kwenye majengo ya Shule ya Sekondari ya Kijitonyama, Dar” alisema Injinia Thomas.

Kabla ya ugawaji wa vyeti kwa wahitimu hao, Kaimu Mtendaji Mkuu wa DTBI Dkt. Daniel Mgori aliwataka wahitimu hao kwenda kuitumia elimu hiyo waliyoipata kutatua changamoto za kijamii kupitia ICT na kuboresha maisha yao.
HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL