×

Waziri Mkuu Majaliwa Atua Morocco Kwa Ziara Ya Kikazi

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  Julai 12, 2021 amewasili nchini Morocco kwa ziara ya kikazi.

Katika uwanja wa Mohammed V jijini Casablanca Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokelewa na Waziri Mwakilishi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika wa Morroco Mohcine Jazouli

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano hususani ya kiuchumi kati ya Tanzania na Morocco.

Katika ziara hiyo Waziri Mkuu ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda na Mkurgenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Japhet Justine.

 

Leave a Comment