×

Rais wa Madagascar Anusurika Kuuawa

Jaribio la kumuua Rais wa Madagascar, Andry Rajoelina limegonga mwamba ambapo watu kadhaa wanaodaiwa kuhusika na jaribio hilo wamekamatwa, mwendesha mashtaka anasema.

 

Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu nchini humo imesema ilifanikiwa kuzuia jaribio hilo jana Jumanne Julai 21, 2021 na watuhumiwa wanashikiliwa kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Watu zaidi ya 6 wakiwemo Raia wawili wa Ufaransa wamekamatwa wakihisiwa kuhusika kupanga njama za mauaji ya Rais huyo.

 

“Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu inaahidi kutoa taarifa kwa kila hatua ya uchunguzi unaoendelea ili kupata mwangaza kuhusu kesi hii,” amesema Mwendesha mashtaka, Berthine Razafiarivony.

 

Katika madhimisho ya siku ya uhuru Juni 26, polisi nchini humo walitangaza kuwa walifanikiwa kuzuia jaribio la kumuua mshauri wa rais Jenerali Richard Ravalomanana.

 

Leave a Comment