
Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Rashid Abdallah Shangazi ambaye ni Mwenyekiti wa Tawi la Simba Bungeni maarufu ‘Wekundu wa Mjengoni’ ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Simba akichukua nafasi ya Barbara Gonzalez, aliyeteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa klabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Simba leo, Shangazi ana uzoefu wa zaidi ya miaka 10 katika medani za kiuongozi katika nyanja za kijamii, kiuchumi na kisiasa. Rashid Abdallah Shangazi kwa sasa si tu Mbunge anayewakilisha Jimbo la Mlalo mkoani Tanga bali pia ni Kamishna wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ni Katibu wa Wabunge wanaowakilisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) na Mwenyekiti wa Wananchama wa Klabu ya Simba Tawi la Bungeni maarufu Wekundu wa Mjengoni.
Written by @erick.evarist cc @hotpot_tz