×

Rigwaride Ra afande- 5

ILIPOISHIA RISASI JUMAMOSI:
Kwa mbali nilijikuta nasisimka kama binadamu. Kama mwanamke, tena mwanamke mwenyewe msichana, kijana kama mimi, damu bado changa! Lakini moyoni nilijiambia…

“Ila mimi ni kiboko…nyumba moja, wanaume watatu tena afadhali ingekuwa siku mbalimbali, leoleo?! Mh!”

Wakati nawaza hivyo, yule mwanaume alinitegesha, nikakaa mkao wa kutengwa…
“Ngo… ngo…afande Mwira,” sauti iliita nje baada ya kugonga mlango…
ENDELEA MWENYEWE SASA…

“Unaona sasa?” nilimsema yule. Kumbe ni afande Mwira…
“Shii,” alinipa ishara kwa mkono kuashiria kwamba nisiseme. Nikakaa kimya. Hapo tayari niko kitandani ujue, tena nimeshategwa!

“Afande Mwira,” ile sauti iliita tena. Safari hii kwa juu kidogo. Niliweza kuitambua kwani nilikuwa makini nayo, nikabaini ni ya yule mbaba wa kwanza kabisa…
“Ee afande,” aliitika afande Mwira sasa…
“Umelala?”

“Hapana, vipi?”
“Tuongee kidogo basi.”
Mimi mapigo ya moyo yalishika kasi, kusikia tuongee kidogo maana si afande Mwira alishasema kuwa, kuna mwenzake ana tabia ya kuingia bila kupiga hodi.
Ingawa mlango ulifungwa lakini nilikuwa nina wasiwasi, hasa nilipojaribu kukumbuka kwamba, huenda nilikuwa natembea kwenye mtego wa wanaume.

Afande Mwira alitoka kitandani, akavaa bukta na kwenda kufungua mlango kisha akasimama mlangoni ili yule mwenzake asiingie…

“Vipi…yaani kuna kabinti bwana nilikuja nako leo…weee! Moto! Kabinti katundu kitandani kama kamechezwa ngoma za kwetu. Kuna siku nitakaleta tena utakaona…kabinti kamjini…pale niko tayari kuteketeza hata mshahara wangu ili nikaoe,” hayo maneno yalikuwa yakitoka kwenye kinywa cha yule mbaba.

Hapo hakuna shaka moja kwa moja kwamba alikuwa ananizungumzia mimi. Nilishangaa sana na misifa hiyo kwangu…kumbe mpango wake ni kunioa, nilichekea moyoni…

“Lo! Kanakaa wapi?” aliuliza afande Mwira ambaye mimi nilikuwa kitandani kwake…
“Kwao.”
Afande Mwira alicheka, mimi mwenyewe pia nilijikuta nikicheka maana sikutegemea jibu hilo. Mtu anaulizwa ‘anakaa wapi?’ anajibu ‘kwao’. Lazima itakuwa kwao, sasa huko kwao ni wapi?

“Mbona unacheka afande Mwira?”
“Nacheka maana umenipa jibu ambalo lipo….”
“Anasema anakaa mitaa ya Wailes kule, kwa baba yake na mama yake.”
Hakuna kubwa waliloendelea kuzungumza, afande Mwira akamuaga mwenzake, akarudi ndani akifunga mlango kwa kitasa taratibu sana…
“Hivi wewe binti, kumbe upo hivyo?” afande Mwira aliniuliza…
“Nikoje?”

“Yaani humu ndani leo ulikuwa kwa wanaume wangapi?”
“Kwani vipi?”
“Huyu afande anasema ulikuwa kwake lakini mimi si nilikusikia ukihema kwa afande mwingine?”

“Labda mwingine. Nyie wenyewe mnaonekana humu ndani mnapenda sana wanawake…”
“Kwani we unakaa wapi?”
“Si Sinza…”

“Sinza! Hukai mitaa ya Wailes wewe?”
“Aka! Wailes napajulia wapi mimi.”
Nilimwona akilainika, akaachana na maswali yake, akazidi kunitega, filimbi ikapulizwa, mchezo ukaanza.

Safari hii niliamua moja, kwamba hata kama nitajiachia vipi sitahemuka tena kwani niligundua nikihemuka ndiyo nasikika na wengine, halafu wananifanyia taiming.
Huyu naye alikuwa wa aina yake, badala ya mimi kuwa na sauti ya muhemko nilimshangaa yeye akaanza kupiga kelele…

“Weee! Weee! Ndiyo nini sasa?” nilimuuliza mwenzangu kwa sauti ya chini…
“Ni kawaida yangu…hii ni kawaida yangu binti,” alinijibu kwa sauti ya juu huku akiendelea na kelele zake.

Ilibidi nisitishe kutoa ushirikiano kwani sasa nilianza kuhisi tunaumbuka wote. Nilijua kelele zake za mahaba zingefika hadi kwenye vyumba vya maafande wengine halafu wangefuatilia kujua kwa afande Mwira kuna nini kinaendelea…
“Sasa inakuaje tena binti…eee! inakuaje?”
Kusema kweli kwa sauti ya juu aliyokuwa anaisema, ilibidi niache kabisa kuendelea na soka…

“Kama uko hivyo siwezi kuendelea na wewe. Unapiga kelele kama ndiyo siku yako ya kwanza bwana,” nilimsema.

Lakini nikahisi dalili kwamba kuna mtu au watu wameshika kitasa cha mlango…
“Wee unasikia…kuna watu mlangoni…kitasa chako kimeshikwa na mtu,” nilimwambia hivyo, ndiyo kidogo kwa mbaaali nikamwona anaacha manjonjo na kukazia macho kwenye mlango.

“Afande Mwira…afande Mwira,” sauti za mtu zaidi ya mmoja zilisikika.
Nilimwona afande Mwira akinyong’onyea kila sehemu ya mwili mpaka kule!
“Eee,” aliitika…
“Mbona unapiga kelele?” hii sasa ilikuwa sauti ya yule mbaba wangu wa mwanzo kabisa…

“Niko sawa jamani…mbona kama tunaanza kufuatanafuatana?”
“Kama upo sawa hebu fungua mlango basi,” ilisema sauti nyingine lakini nayo niliikumbuka ni ya yule afande wa pili aliyenikatia nusu laki.
Nilijua kimenuka, msichana naumbuka. Tena mbaya zaidi naumbukia kwa mtu niliyeamua kwenda naye bureee! Kwa kumwonea huruma…
“Fungua bwana…inasemekana uko na kale kabinti…”

Leave a Comment