×

Wajane Wadai Kuporwa Eneo Lao Wamlilia Mama Samia Aingilie Kati

Wajane wa marehemu Amiri Mrisho, Bi Anseline Mrisho na Amina Mrisho (kulia) walipokuwa eneo la tukio.

 

 

Wajane wa Marehemu Amiri Mrisho Bi. Anseline Mrisho na Amina Mrisho wameangua kilio hadharani na wakimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kuokoa eneo lao wanalodai linataka kunyang’anywa baada ya kuibuka mgogoro.

Wakizungumza na wanahabari wajane hao walisema eneo hilo lililopo Soko la Tazara, Dar, lilikuwa likimilikiwa kihalali na marehemu mume wao lakini alipofariki walitokea matajiri na kumlaghai mmoja wa watoto wa marehemu na kufanya nae biashara ya kuwauzia eneo hilo bila kuwashirikisha wao kama wajane wa marehemu.

Sehemu ya wapangaji wanaofanyia shughuli zao eneo hilo wakiwa katika taharuki na mabango yao baada ya kupata taarifa za eneo hilo kuchukuliwa na mmiliki mwingine nao kutojua hatima yao.

 

 

Wameendelea kusema baada ya kubaini kuwa eneo waliloachiwa na marehemu mume wao limeuzwa walianza kuhangaikia suala hilo kisheria lakini wamedai kugonga mwamba kila walipokimbilia.

“Hili ni eneo letu jamani ametuachia marehemu mume wetu mimi na huyu mjane mwenzagu lakini watu wenye pesa wametumia pesa zao vibaya kwa kumshawishi mmoja wa watoto zetu na kulipora eneo letu.

“Wanatuambia eneo hilo limeuzwa na pesa zetu wametuwekea benki hata hivyo tulipofuatilia hizo pesa tukagundua kuwa ni ndogo mno ukilinganisha na thamani ya hili eneo letu.

Wajane hao wakiwa na wapangaji wao ambapo sasa hawajui jinsi watakavyo malizana nao.

 

 

“Hata hivyo kama ni eneo kuuzwa kwanini huyo mtoto wetu hakutushirikisha hata kwenye kupanga bei, tunaonewa jamani. “Tunakuomba rais wetu,mtetezi wa wanyonge, Mama Samia Suluhu sisi ni wanawake wanyonge hapa tulipo tumeachwa wajane tunaomba hutusaidie ufumbuzi wa huu mgogoro. “Hivi tunavyoongea tumeshapewa notisi ya kuhama ili eneo letu ambapo tumepewa siku 30 baada ya hapo hizi frem za maduka na kila kilichopo hapa kitakuwa chini ya huyo aliyeuziwa.

Mmoja wa watoto wa marehemu akizungumza na wanahabari kuhusiana na tukio hilo.

 

 

“Hili eneo sisi ndiyo lililokuwa likitulea baada ya kifo cha mume wetu sasa sijui tutaishije” walisikika wakilia wajane hao wakati wakiomba msaada kwa Rais Mama Samia.

Leave a Comment