
WAKATI mchezo wa Ligi Kuu Bara ukipigwa jana kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, Yanga walionekana kuifunika Simba. Kabla mchezo huo haujaanza mashabiki wa Yanga walikuwa wengi zaidi kuliko wale wa Simba ikiwa ni nadra sana hali hiyo kutokea.
Mpaka majira ya saa saba mchana, majukwaa ambayo huwa yanakaliwa na Yanga yalikuwa yameshajaa, huku majukwaa ambayo yalikuwa yanakaliwa na Simba yenyewe yalikuwa bado yana mapengo mengi na mashabiki baadhi wa Yanga walisogea kukaa hapo.
Hali hii ilikuwa inatokea haya nje ya uwanja ambapo mashabiki waliokuwa wamevaa jezi za Yanga walikuwa wengi zaidi kuliko wale wa Simba.
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam