KLABU ya Barcelona inajiandaa kumpa mkataba mpya mshambuliaji wake Lionel Messi kabla ya kuvaana na Juventus.
Barcelona watavaana na Juventus wiki ya kwanza ya mwezi ujao na wanataka mchezaji huyo awe ameshasaini mkataba kabla ya mchezo huo.
Messi ambaye kwenye maisha yake yote amekuwa akitumika kwenye kikosi cha Barcelona hivi karibuni alisema kuwa yupo tayari kusaini mkataba mpya na timu hiyo ya Hispania.
Klabu ya Barcelona imeshasema kuwa mazungumzo kati ya mchezaji huyo na klabu yamekamilika na kila kitu kuhusu mkataba wake kipo tayari.
Kwa mujibu wa taarifa ya Gazeti la Daily Mail, mchezaji huyo atasaini mkataba huo mpya mwanzoni mwa mwezi ujao tayari kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Hispania.
Barcelona wanataka kuona mchezaji huyo anatumika kwenye mchezo dhidi ya Juventus ambayo itakuwa na staa Cristiano Ronaldo.
Ronaldo naye bado hajawa na uhakika wa asilimia 100 wa kubaki kwenye timu hiyo, lakini ameshakiri kuwa atakuwepo kwenye mechi hiyo