
NAELEZWA kuwa mshambuliaji wa Namungo, Stephen Sey, raia wa Ghana anatembea na mkataba wa Yanga ambao ametumiwa ausome na kama akiridhika aweze kusaini.
Taarifa kutoka kwa mtu wa karibu na Sey alithibitisha uwepo wa mazungumzo baina ya nyota huyo wa zamani wa Singida United na Yanga na kudokeza kuwa kama mambo yatakuwa sawa, jamaa atadondoka saini.
Kikizungumza na Championi Jumatatu, chanzo cha ndani cha uhakika kimesema kuwa: “Sey yupo kwenye mazungumzo na Yanga, kwa sababu walionyesha nia ya kutaka kuwa naye tangu dirisha dogo, ila kwa sasa wanaonekana kuwa wapo sehemu nzuri zaidi ya kufikia muafaka, tayari walimpa mkataba aupitie, nafikiri akiwa tayari mambo yataisha.”
Alipotafutwa Sey mwenyewe ili kusikia anasemaje alisema: “Kwa sasa nipo nyumbani Ghana kwa mapumziko, sijui chochote, tusubiri tuone.”
ISSA LIPONDA, Dar es Salaam.