×

Kesi ya Mbowe Yaahirishwa, Wafuasi Chadema Wasombwa

POLISI jijini Dar es Salam wamewatawanya wafuasi wa Chadema ambao walikuwa wamekusanyika nje ya mahakama ya Kisutu kufuatilia kesi ya mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Alhamisi, Agosti 5, 2021.

 

Kesi hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa kwa nia ya mtandao hata hivyo imeahirishwa kutokana na changamoto za kimawasiliano. Mbowe anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo kesho asubuhi kuendelea na kesi hiyo.

 

Awali wafuasi wa Chadema walionekana nje ya mahakama hiyo wakiwa na mabango yanayosomeka: ‘Mbowe sio gaidi’ na pia walikuwa wakipaaza sauti na kusema, ‘katiba mya sio ugaidi’.

Hata hivyo polisi wamewatawanya kwa nguvu wafuasi hao na baadhi yao kukamatwa. Mawakili wa Mbowe wakiongozwa na Peter Kibatala, wapo mahakamani hapo lakini mteja wao ni mahabusi katika gereza la Ukonga.

 

Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kufadhili vitendo vya kigaidi. Wakosoaji wa serikali ikiwemo Chadema pamoja na mashirika ya haki za kibinadamu wanaichukulia kesi hiyo ni ya kisiasa na kushinikiza serikali imwachie huru mwanasiasa huyo.

Hata hivyo polisi wamekanusha madai hayo na kwamba wanasema wana ushahidi wa kutosha kwamba Mbowe alitenda makosa hayo na kutaka mahakama iachwe itekeleze wajibu wake.

 

Mawakili wa Mbowe wakiongozwa na Peter Kibatala , wapo mahakamani hapo lakini mteja wao ni mahabusi katika gereza la Ukonga. Mbowe anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu uchumi na kufadhili vitendo vya kigaidi.

Wakosoaji wa serikali ikiwemo Chadema pamoja na mashirika ya haki za kibinadamu wanaichukulia kesi hiyo ni ya kisiasa na kushinikiza serikali imwachie huru mwanasiasa huyo.

 

Hata hivyo polisi wamekanusha madai hayo na kwamba wanasema wana ushahidi wa kutosha kwamba Mbowe alitenda makosa hayo na kutaka mahakama iachwe itekeleze wajibu wake.

 

“Teknolojia imefeli hivyo tumeshindwa kufanikisha mchakato huo kwa sababu kumekuwa na mawasiliano hafifu kati ya video conference facility za hapa katika Mahakama ya Kisutu na Gereza la Ukonga na tumekubaliana kwamba kesho washitakiwa waletwe mahakamani.

 

“Upande wa Serikali na Magereza imeshindwa kumtela Mhe. Freeman Mbowe⁩ leo kwa sababu zao lakini pia tumeshindwa kuendelea na kesi kwa njia mtandano hivyo Mahakama imeamuru kesho ataletwa Mahakamani ili kuendelea na Shauri,” Wakili Peter Kibatala.

 

“Mahakama imeamuru kesho Mhe. ⁦Freeman Mbowe aletwe Mahakamani hivyo nitoe wito kwa watanzania wote wafike Mahakama ya Kisutu kufatilia shauri hili, kwende Mahakamani sio kosa kisheria,” ⁦amesema John Mnyika.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment