×

Mwili wa Waziri Kwandikwa Wawasili Nyumbani Kwao

MWILI wa aliyekuwa mbunge wa Ushetu Wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga Elias Kwandikwa ,tayari umewasili nyumbani kwake kijijini Butibu_Kinamapula katika halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama na kuingizwa ndani ya nyumba yake kusubiria taratibu za mazishi.

 

Kwandikwa alikuwa pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa ,alifariki siku chache zilizopita akiwa jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

 

Tayari Viongozi mbalimbali wamewasili Kijijini hapa akiwemo Mkuu wa Majeshi CDF Venance Mabeyo na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dr. Philemon Sengati. Mwili wa Kwandikwa umesafirishwa kwa helkopita ya jeshi hadi kijijini hapo.

 

Marehemu Elias Kwandikwa atazikwa kesho August 9 hapahapa Kijijini kwao Butibu na shughuli hiyo inatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 

Leave a Comment