
Polisi nchini Zimbabwe wanachunguza kifo cha msichana mwenye umri wa miaka 14-kilichotokea wakati anajifungua, kesi hiyo imeibua hisia mbalimbali miongoni mwa wananchi na wanaharakati wa haki za binadamu. Memory Machaya ameripotiwa kufariki mwezi uliopita katika madhabau mashariki mwa mji wa Marange.
Kesi hiyo imeelezewa kuwa ni unyanyasaji wa watoto, binti huyo aliripotiwa kulazimishwa kuacha shule ili aolewe. Umoja wa Mataifa umetaka serikali kuidhinisha kuwa mimba za utotoni ni uhalifu na kusitisha utamaduni huo.
Shirika hilo limesema wasiwasi wake mkubwa na kulaani vikali ripoti kuhusu kifo cha binti huyo. Shirika hilo limesema “linatoa maelezo juu ya wasiwasi wake mkubwa” na “limelaani vikali” ripoti zinazoelezea jinsi kifo kilivyojitokeza.
“Hali iliyopo sasa ya kutotatua kesi za unyanyasaji kwa wanawake na wasichana nchini Zimbabwe, zikiwemo kesi za ndoa za utotoni, haiwezekani kuendelea kupuuzwa,” taarifa ya UN ilieleza siku ya Jumamosi. Kifo cha binti huyo kilichotokea Julai 15, kimetoa angalizo juu ya mimba za utotoni katika kanisa la Zimbabwe Apostolic ,ambalo limekuwa linakataa dawa na tiba za hospitalini.
Familia yake ilisema mtoto alipona na alijifungua salama, vyombo vya habari vya ndani vimeripoti. Mazingira ambayo yalipelekea kifo chake kuchunguzwa na polisi na tume ya jinsia nchini humo.
Baadhi ya watu waliandika maombi yao mtandaoni kwa kutaka haki itendeke juu ya kifo cha binti huyo Memory Machaya” mpaka sasa saini za watu zaidi ya 57,000 zinataka haki ipatikane. Mwanaharakati wa Zimbabwe wa kutetea haki za wanawake bi.
Everjoice Win alisema” ni wakati muafaka kwa watu kuweka msukumo kwa walio madarakani kuweka sheria mpya. Wanawake na wasichana hawaonekani kama binadamu waliokamilika wenye haki … na kuwa na mamlaka ya miili yao” aliandika kwenye Twitter. Kisheria, wasichana wa Zimbabwe wanaruhusiwa kuolewa wakiwa na miaka 18, wakati miaka 16 kuwa na idhini ya kujamiiana.
Lakini baadhi ya familia wanaamini kuwa ndoa za utotoni zina manufaa ya kifedha. Mabinti wengi wanaoolewa wakiwa wadogo wana matumaini kuwa ndoa itawapatia fursa ya kwenda shule. Hata hivyo , mabinti hao huishia kupata mimba mara tu baada ya kuolewa na hivyo kubaki kuwa mama wa nyumbani.