×

Vodacom Tanzania Yasambaza Mtandao 4G Kwenye Vituo Zaidi ya 1800

Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi.Rosalynn Mworia wakati wa uzinduzi wa Kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI

 

 

Kampuni ya Mtandao wa Vodacom Tanzania mpaka Sasa umeshapeleka mtandao wa 4G kwenye vituo zaidi ya 1800 na katika mwaka huu wa fedha wamezindua vituo 400 vya 4G Tanzania nzima.

 

Ameyasema hayo leo Mkurugenzi wa Mawasiliano, Bi.Rosalynn Mworia wakati wa uzinduzi wa Kampeni mpya ya KIMBIZA NA 4G YA UKWELI uliofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam.

Sehemu ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio.

 

 

Akizungumzia katika uzinduzi huo, Bi.Rosalynn amewataka wale ambao hawajapata fursa hiyo awaweze kutumia mtandao wa Vodacom ili waweze kuunganishwa na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wa 4G wenye kasi zaidi na kuweza kufurahia huduma hiyo katika maeneo mengi ambayo mwanzo hayakuweza kufikiwa kwa urahisi.

 

 

“Uzinduzi huu unaenda kugusa Maisha yetu tofautitifauti, Kuna wafanyabiashara wadogowadogo, wafanyabiashara wakubwa, wakina Mama lishe wanaweka vitu vyao kwenye mitandoa ya kijamii, hii yote imewezakana kutokana na data”. Amesema Bi.Rosalynn.

Leave a Comment