×

PSG Kuuza Wachezaji 10 Kikosi cha Kwanza Kuziba Pengo Mkwanja wa Messi

RASMI aliyekuwa nahodha wa timu ya Barcelona Lionel Messi sasa ni mali ya PSG ya Ufaransa 🇫🇷. Nyota huyo ambaye amedumu kwa muda wa miaka 21 ndani ya Barcelona amesaini dili la miaka miwili akiwa ni mchezaji huru baada ya mipango yake kusalia Barca kwa miaka mitano ijayo kugonga mwamba.

Messi amechagua jezi namba 30 ambayo amekabidhiwa aliyoanza kuitumia alipokuwa Barcelona ndani ya Nou Camp akiwa kinda ambapo kandarasi yake ndani ya PSG kikiwa na kipengele cha kuongeza hadi Juni 2024.

 

Mshindi huyo mara sita wa tuzo ya Ballon d’Or anaungana na mshikaji wake Neymar Jr waliyefanya naye kazi nyakati fulani ndani ya Barcelona.

Messi mwenye umri wa miaka 34 amemaliza dili hilo ambalo atalipwa paundi milioni 25 kwa mwaka (sawa na Tsh bilioni 80.362) baada ya kukatwa kodi pamoja na bonasi.

Hii imekuja baada ya kuachana na klabu yake ya Barcelona aliyoitumikia kwa miaka 18 kutokana na mkataba wake wa miaka mitano kushindikana kutokana na sheria za La Liga licha ya Messi kukubali kukatwa asilimia 50 ya mshahara wake.

 

Messi anakwenda kuungana na swahiba wake, Neymar Jr aliyekuwa naye Barca miaka michache iliyopita, pamoja na Kylian Mbappe na Mu-Argentina mwenzake, Angel Di Maria katika kikosi hicho kinachonolewa na Mauricio Pochettino.

Paris St-Germain italazimika kuuza hadi wachezaji 10 wa kikosi cha kwanza ili kusawazisha mahesabu yao baada ya kumsajili a Lionel Messi, 34. Kiungo wa Senegal, Idrissa Gueye, 31, kiungo wa Hispania, Ander Herrera, 31, na 28 mshambuliaji wa zamani wa Argentina, Mauro Icardi ni miongoni mwa wale ambao wanaweza kuuzwa.

Leave a Comment