×

Ben Pol Mwanaume Kuomba Talaka si Dhambi

Msanii wa Bongofleva, Ben Pol ambaye hivi karibuni alimwagana na mkewe Anerlisa amesema alitamani kuwanasa watu waliokuwa wakimkejeli kutokana na uamuzi wake wa kwenda mahakama kufungua shauri la talaka.

 

Akipiga stori na IJUMAA Wikienda wiki chache baada ya kuachana na mkewe huyo kutoka nchini Kenya, alisema Watanzania wengi hawaijui  sheria.

Alisema wanawake ndio waathiriwa wakubwa zaidi kwa sababu talaka yoyote inayotolewa nje ya mahamaka haitambuliki.

 

“Zile talaka tatu hazina mchongo, chombo chenye mamlaka halali ya kutoa talaka ni mahakama kwa upande wa Tanzania.

 

Kama mwanamke au mwanaume akisema hii indoa siitaki anaenda kufungua shauri ya talaka mahakamani.“Ile si kuomba talaka, ni kufungua shauri kuwa jamani hii ndoa hainifai tena, na mahakama ndio chombo pekee,” alisema Ben Pol

Leave a Comment