×

Wanamgambo wa Taliban Waingia Kabul

WANAMGAMBO wa Taliban wameanza kuingia katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul, baada ya kuidhibiti miji mingine mikubwa nchini humo.

 

Hatua hiyo inatajwa kuwa ishara ya wazi ya wapiganaji hao kulidhibiti kijeshi taifa la Afghanistan, lakini msemaji wa kundi hilo amesema wamewaamuru wapiganaji wake wasiingie katikati ya jiji hilo.

 

Amri hiyo imetolewa baada ya wakaazi kusema wamewaona wanamgambo wakiingia katika viunga vya pembezoni mwa jiji hilo bila makabiliano yoyote.

 

Hilo linatokea baada ya kufanikiwa kuudhibiti mji muhimu wa Jalalabad huko mashariki mwa Afghanistan kwa sasa ni mji wa Kabul pekee ndiyo umesalia chini ya udhibiti wa serikali ya taifa hilo.

 

Kati ya majimbo 34 ya Afghanistan, Taliban inaidhibiti miji mikuu yake takribani 25 miji yote hiyo imedhibitiwa katika muda wa siku kumi pekee.

 

Wakati wanamgambo hao wakisonga mbele mataifa kama Ujerumani, Ufaransa yanaendelea na juhudi za kuwaokoa maafisa wao ambao bado wapo nchini Afghanistan.

Leave a Comment