×

Waliogombania Ndege Afghan Kutua Uganda

 

SERIKALI ya Uganda imesema kuwa itawachukua wakimbizi 2000 wa Afghanistan wanaokimbia mzozo nchini mwao – kufuatia ombi la Marekani. Siku ya jana mamia ya Waafghanistan ambao walionekana uwanja wa ndege wa nchi hiyo wakipanda ndege ya jeshi la Marekani kukimbia mzozo unaoendelea nchini humo.

Hii inafuatia hatua ya wanamgambo wa Taliban kuchukua uongozi wa nchini hiyo wikendi iliyopita baada ya serikali iliyokuwa madarakani kuanguka.

Uganda imepongezwa kimataifa kutokana na sera yake ya kuwakaribisha wakimbizi.

Kundi la kwanza la karibu Waafghanistan 500 linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe saa chache zijazo.

Waziri wa Wakimbizi wa Esther Anyakun ameiambia BBC kwamba Rais Museveni amekubali kuwachukua jumla ya wakimbizi 2000 raia wa Afghanistan – kufuatia ombi la Marekani.

Aliongeza kuwa watakapofika watafanyiwa vipimo vya corona na kuwekwa karantini. Vifaa na gharama zote zitashughulikiwa na Serikali ya Marekani.

Uganda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwapokea watu wanaotoroka ghasia nchini Afghanistan.

Leave a Comment