×

Ukutawa Chuma Umekamilika

NI rasmi sasa klabu ya Simba imemtangaza beki wa Kimataifa raia wa DR Congo, Henock Inonga Baka kuwa mchezaji wao mpya kuelekea msimu ujao wa 2021/22.

 

Baka mwenye umri wa miaka 26, sasa ataungana na mabeki Joash Onyango, na Pascal Wawa kukamilisha ukuta wa chuma wa Simba kwa msimu ujao ambao pia una wazawa Kennedy Juma na Ibrahim Ame.

 

Mkongomani huyo amejiunga na Simba kama mchezaji huru akitokea klabu ya DC Motema Pembe, ya kwao DR Congo aliyoichezea tangu mwaka 2018.

 

Baka anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na kutambulishwa rasmi na Simba kuelekea msimu ujao ambapo mpaka sasa wachezaji wanne waliotangazwa kujiunga na Simba ni wa kimataifa na mzawa mmoja.

 

Nyota wengine ambao tayari wametambulishwa ni; Wamalawi Peter Banda na Duncan Nyoni, Msenegali Pape Ousmane Sakho, huku mzawa akiwa ni Yusuph Mhilu.

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

Leave a Comment