×

Yanga Hakuna Kulala Morocco, Nabi Aaanza Dozi Ya Kibabe

MARA baada ya kikosi cha Yanga kutua nchini Morocco, haraka Kocha Mkuu wa timu hiyo, Mtunisia Nasreddine Nabi alianza program ya mazoezi.


Hiyo ikiwa ni siku moja tangu
kikosi hicho kiwasili Morocco na tayari kwa ajili ya kambi ya siku kumi waliyopanga kuiweka nchini huko.

 

Yanga hivi sasa wapo katika maandalizi ya nguvu kuhakikisha timu hiyo inafanya vema katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika watakayoshiriki.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela ambaye ameongozana na msafara huo alisema kuwa kikosi hicho kilianza program ya mazoezi na pamoja jana Jumanne.

 

Mwakalebela alisema kuwa, timu hiyo ilianza mazoezi jana asubuhi na jioni chini ya Nabi ambaye ndiye aliyekipokea kikosi hicho hapo Morocco.

Aliongeza kuwa kwa kipindi hicho watakachokaa Morocco watafanya mazoezi mara mbili kwa siku kwa ajili ya kutengeneza fitinesi ya wachezaji wake wote.

 

“Wachezaji wote 28 wapo kambini Morocco kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya ambao tumepanga kufanya vema.

“Mazoezi tulianza leo (jana) asubuhi kwa kufanya mazoezi ya asubuhi na jioni ambayo tutaendelea nayo tena kesho kwa kufanya program hizo mbili.

 

Kocha ndiye aliyependekeza tufanye program hizo lengo ni kutengeneza fitinesi na muunganiko wa wachezaji wapya na zamani,” alisema Mwakalebela

Leave a Comment