×

Basi la Sauli Lapata Ajali Kibaha, Wanne Wajeruhiwa

WATU wanne wamejeruhiwa na wengine 40 kunusurika baada ya kutokea ajali ya basi la kampuni ya Sauli eneo la Picha ya Ndege Kibaha mkoani Pwani.

 

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu Agosti 23, 2021 saa 6:45 asubuhi baada ya dereva wa basi hilo ambaye jina lake halikupatikana wakati huo kulielekeza pembezoni mwa barabara ili kukwepa kugongana uso kwa uso kwa uso na lori lillokuwa likitokea mbele yake.

 

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema kuwa dereva wa basi hilo alikuwa akilipita gari lililokuwa mbele yake na baada ya kufanikiwa aliona lori la mchanga ndipo aliamua kulikwepa.

 

“Alikuwa anaovateki gari lililokuwa mbele yake na baada ya kulipita aliona lori linakuja mbele yake akalielekeza pembezoni mwa barabara basi hilo na likachegama,”alisema.

 

Alisema kuwa majeruhi hao wamewahishwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi ambapo walipatiwa matibabu kisha kuruhusiwa.

 

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Leave a Comment