×

Tanzia: Maalim Seif Azzan Afariki Dunia

Maalim Seif Mohamed Azzan amefariki Dunia usiku wa kuamkia leo Kisiwani #Pemba. Alikuwa miongoni mwa Waasisi wa Harakati za Mageuzi na kuwaunganisha Wazanzibari, kupigania Haki na #Demokrasia ya Vyama vingi.

 

Seif Azzan amewahi kuwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoka Jimbo la Pandani katika Bunge la kwanza la Vyama vingi Mwaka 1995-2000. Mpaka mauti inamkuta alikuwa Afisa Utawala wa ACT-Wazalendo, Kanda ya Pemba.

 

Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika; “Mzee wetu Maalim Mohamed Azzan ametangulia mbele ya Haki. Anapumzishwa Leo baada ya salat alasiri huko Pemba. Alikuwa Mbunge katika BUNGE la kwanza la Mfumo wa Vyama vingi nchini 1995-2000. Alikuwa msaidizi wa Karibu na mwaminifu Kwa Mzee wetu Marehemu Maalim Seif Sharif.”


Leave a Comment