×

SpotXtra Lagawa Tiketi Bure za Siku ya Wananchi kwa Wasomaji Wake

Afisa Masoko wa Global Publishers watoaji wa gazeti la Sport Xtra, Juma Johanes (kulia) akiwa na msomaji aliyemkuta Uwanja wa Benjamini Mkapa akiwa na gazerti hilo.

 

 

 

TIMU gazeti la Sport Xtra, leo imegawa tiketi kwa wasomaji wake kwa ajili ya kuingia kwenye siku ya Wananchi inayofanyika Uwanja wa Benjamini Mkapa Dar.

Afisa Masoko wa Global Publishers, Juma Johanes (kushoto) akimkabidhi tiketi ya kuiona Siku ya Wananchi msomaji aliyemkuta na gazeti la Sport Xtra.

 

 

Zoezi hilo liliongozwa na Afisa Masoko wa Kampuni ya Global Publishers, Juma Johanes na kuwaacha mashabiki hao wakifurahia uhondo wa Sport Xtra na hafla hiyo.

Shabiki huyu akitoa mikogo baada ya kupewa tiketi na timu ya Sport Xtra.

Katika zoezi hilo timu ya Sport Xtra ilipofika Uwanjani hapo ilianza kugawa kwa wasomaji wake iliyowakuta na gazeti hilo.

Shabiki wa Yanga akifurahia gazeti ya Sport Xtra.

 

Kikosi hicho kilizungumza mawili matatu na wasomaji hao na kuwauliza maswali kuhusiana na gazeti Sport Xtra pamoja na magazeti mengine yanayotolewa na Global Publishers ambapo waliojibu vizuri walijizolea tiketi hizo.

Mashabiki wa Soka wakiwa kwenye harakati za kuingia uwanjani.

 

 

Magazeti mengine yanayotolewa na Global Publishers ni pamoja na Championi, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS/ GPL     

Leave a Comment