×

Nabi Amkabidhi Jukumu Zito Fei Toto

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nassredine Nabi, amempa majukumu mazito kiungo mshambuliaji wake Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa kumtaka kuongeza uwezo wa kupeleka mashambulizi sambamba na kuichezesha timu muda wote wa mchezo.


Septemba 18 mwaka huu,
Yanga itashuka dimbani kukabiliana na Rivers United ya nchini Nigeria, katika mchezo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, jambo ambalo Nabi limemlazimu kumpatia majukumu hayo Fei Toto.

 

Chanzo chetu kutoka kambi ya Yanga, iliyopo Avic Town Village, Kigamboni jijini Dar es Salaam, kimeweka wazi kwamba, kwa sasa Nabi anafanya kila liwezekanalo ili kuhakikisha wachezaji wake popote walipo wanatumia muda wao kufanyia maagizo yake kazi.

 

“Pamoja na Fei Toto kuwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, bado kocha wetu Nabi ameamua kumpatia majukumu hukohuko ili ahakikishe anaporudi aweze kutengeneza muunganiko ndani ya timu kama mchezeshaji wa timu.

 

“Kocha Nabi ametoa majukumu hayo kwa wachezaji wote ambao wamejiunga na timu zao za taifa, kwani anaamini kwakuwa wanajitambua kila mmoja kwa nafasi yake atatumia muda wake kutekeleza maagizo aliyowapatia,” kilisema chanzo hicho.

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

Leave a Comment