Washereheshaji wa bahati nasibu hiyo wakiongozwa na MC Chaku wakionesha ‘machejo’ wakati wa kuchezesha droo ya zawadi za awali eneo la Kawe Dar.
MC Chaku (kushoto) akimwangalia msomaji wa magazeti ya Global ambaye ni mkazi wa Kawe akikata kuponi kwenye gazeti lake ili kushiriki shindano la Shinda Nyumba na Global Publishers.
Wasomaji wa magazeti ya Global eneo la Kawe wakiyachangamkiana kuyanunua magazeti kwa muuzaji (katikati) ili kushiriki bahati nasibu hiyo.
Wananchi wa Kawe wakijaza kuponi eneo la stendi ya daladala ya Kawe ili kushiriki bahati nasibu hiyo .
Zoezi la kuweka kuponi kwenye ndoo iliyoandaliwa kwa ajili ya bahati nasibu hiyo likifanyika kwa wakazi wa Kawe Dar.
Zoezi la kuweka kuponi zilizokuwa zimekatwa kutoka kwenye mazeti ya Global ili kushiriki bahati nasibu likifanyika.
…Kuponi zikiendelea la kuweka ndani ya ndoo huko Kawe.
Baadhi ya wananchi waliopata hamasa ya kununua magazeti na kujaza kuponi ili kushiriki Bahati Nasibu wakijaza sehemu inayowahusu kuijaza.
Mmoja wa wanenguaji katika shindano hilo akionesha sarakasi kama moja ya burudani za utangulizi wa Bahati Nasibu hiyo.
MC Chaku (kushoto) akimwangalia mwanamama mkazi wa Kawe akichanganya kuponi
Mwanamama huyo akichukua kuponi ili isomwe kwa ajili ya mshindi wa Bahati Nasibu ili apate fulana ambapo kuponi hizo zinaendelea pia kuingia katika droo ya Shinda Nyumba.
Mshindi kwenye droo za awali za kushinda fulana (wa pili kushoto) akiwa amevaa tayari fulana yake.
Mr. Championi akimkabidhi mshindi wa awali fulana katika droo iliyochezeshwa jana maeneo ya Kawe
Washindi wa awali wa kofia zilizoandikwa Shinda Nyumba wakiwa katika picha ya pamoja na Mr. Championi.
Burudani ikipamba moto wakati wa shughuli hiyo.
Wakazi wa eneo la Ubungo Darajani wakichangamkia kununua gazeti kutoka kwa muuzaji ili kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Wakazi wa eneo la Ubungo eneo la kituo cha mabasi ya kwenda mikoani wakijaza kuponi na kutumbukiza kwenye ndoo maalum kwa ajili ya kushiriki Bahati Nasibu hiyo.
Gazeti zikichangamkiwa kununuliwa eneo la Ubungo ilipokuwa ikifanyika Bahati Nasibu ya awali ya kushinda fulana ambapo kuponi hizo zinaendelea kuingia katika bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Kuponi zikiendelea kuingizwa kwa ajili ya kushiriki Bahati Nasibu hiyo .
Mmoja wa abiria aliyekuwa akisubiri usafiri Kituo cha Mabasi, Ubungo akiweka kuponi yake kwa ajili ya kushiriki Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba.
Ofisa usambazaji wa Global Publishers, Jordan Ngowi (kulia) akiwasaidia wasomaji kukata kuponi ili washiriki Bahati Nasibu hiyo.
Wasomaji wa magazeti ya Global wakisoma ukurasa ulioandikwa kipengele cha kushiriki Bahati Nasibu hiyo eneo la Ubungo.
Mshindi wa Bahati Nasibu ya awali (wa pili kulia) aliyeshinda fulana akiwa ameivaa baada ya kupewa na Mr. Championi. Kuponi hizo zitashiriki pia katika bahati nasibu ya Shinda Nyumba.
Mshindi wa Bahati Nasibu (katikati) akiwa na zawadi yake kutoka kwa Mr. Championi eneo la Ubungo baada ya kuchezeshwa droo ya awali.
Mshindi aliyejipatia fulana akimpa mkono Mr.Championi.
Mwanadada Iqra Mdoen akichanganya kuponi kwa ajili ya mshindi wa bahati nasibu wa zawadi za awali.
Mshindi wa awali wa bahati nasibu akiwa amevalishwa kofia na Mr. Championi baada ya kuchezeshwa bahati nasibu.
Wakazi wa eneo la Mabibo Soko la Ndizi wakiweka kuponi zao kwenye ndoo maalum ya kuchezesha bahati nasibu.
Wakazi wa eneo la Mabibo wakiendelea kuweka kuponi zao kwenye ndoo.
Baadhi ya wakazi wa Keko Dar wakijaza kuponi za kushiriki bahati nasibu hiyo.
JUZI baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, kuzindua Bahati Nasibu iliyoanza Ijumaa ya Shinda Nyumba linaloendeshwa na Global Publishers, kampuni inayochapisha gazeti la michezo la Championi na magazeti pendwa ya Uwazi, Amani, Ijumaa, Risasi na Ijumaa wikienda, jana wakazi wa jiji la Dar es Salaam walizindua shindano hilo kwa kishindo baada ya kujinyakulia zawadi mbalimbali za fulana na kofia baada ya kuchezeshwa bahati Nasibu ya awali.
Miongoni mwa zawadi walizozipata ni fulana na kofia zilizoandikwa Shinda Nyumba na Global Publishers baada ya kununua magazeti na kukata kuponi zilizochezeshwa mbele ya wasomaji hao wa maeneo ya Kawe, Ubungo, Mabibo Soko la Ndizi na Keko.
Katika Bahati Nasibu hiyo msomaji anatakiwa kununua nakala moja au zaidi ya magazeti na kukata kuponi moja iliyo katika magazeti hayo kisha kujaza jina lake kamili na anuani yake na kutuma kwa njia ya posta au kuipeleka moja kwa moja katika ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga-Mwenge ama kuzipeleka kwa mawakala wa kuuza magazeti popote nchini.
Aidha Bahati Nasibu hiyo inatarajiwa kuendeshwa kwa muda wa miezi sita ambapo nyumba inayoshindaniwa iliyojengwa huko Salasala, Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ikiwa na samani za ndani, itatolewa mwishoni mwa mchezo.
Kwa upande mwingine, droo nyingine ndogo zitaendelea kutolewa kila mwezi, ambapo kutatolewa simu mpya za kisasa, runinga na ving’amuzi.
Katika shindano hili, watu walio chini ya umri wa miaka 18 na wafanyakazi wa Global Publishers na ndugu zao, hawaruhusiwi kushiriki.
Stori: Denis Mtima/GPL