
MCHEKESHAJI aliyeibuka hivi karibuni na ku trend kwenye mitandao ya kijamii, Cholo Boy, ametinga katika studio za Global Radio na kufunguka ishu mbalimbali kuhusu kazi yake na maisha yake kwa ujumla.
Akipiga stori na +255 Global Radio, Cholo amesema imemlazimu kusafiri kutoka Songea mpaka dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta maisha na kuikuza sanaa yake baada ya kuona sehemu alipokuwa kuna watu walikuwa hawamkubali hivyo walimdharau na kumfanya ajione mnyonge.
“Baada ya kumaliza elimu ya msingi nilikuwa nikifanya kazi ya ukondakta kwenye magari ya Peramiho huko nyumbani Songea. Lakini kuna watu walikuwa hawanipendi walinichukia sana, wakiniona tu wanakasirika hata kwenye gari wanakataa kupanda.
“Ilifika wakati nikikatisha mtaani watu wananidharau, wananifanya kuwa kitishio cha watoto wao. Mfano ukikuta mtoto analia unasikia anaambiwa “nyamaza nitakutishia yule pale” kwa kweli iliniumiza sana. Nadhani walikuwa wanafanya hivyo kutokana na maumbile yangu nilivyo,” amesema Cholo.