
MSANII wa comedy anayechipukia Bongo, Cholo Boy amesema kwa sasa hataki mwanamke kwa sababu mademu wengi wa Bongo wanataka pesa na kiki badala ya mahusiano yenye manufaa katika maisha yao.
Cholo amesema hayo wakati akipiga stori na Kipindi cha Kata Mbunga kinachoruka kupitia +255 Global Radio kila Jumatatu hadi Ijumaa.
“Kwa sasa sihitaji mahusino ya kimapenzi na mwanamke yeyote, walikuwa wapi zamani mpaka wajisogeze sasa hivi baada ya kuniona nimekuwa staa, au wanataka kiki kupitia kwangu, sitoi kiki kwa mtu mimi.
“Nasema hivyo kwa sababu huko nyuma nikiwa nyumbani niliwahi kumtongoza msichana mmoja ambaye nilimpenda sana, lakini akanikatalia akasema ‘naanzaje kutoka na wewe? Mwanaume mzee, nitawaambiaje marafiki zangu kwamba natoka na wewe? Si aibu hii? Kuanzia hapo nikakata tamaa ya kutongoza tena.