
Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla ametoa wiki moja kwa wafanyabiashara ndogo wanaofanya biashara kwenye njia za watembea kwa miguu kuondoka maeneo hayo.
Sambamba na hilo ametoa maagizo kwa Wakuu wa Wilaya, kuratibu mahali maeneo watakayokwenda wafanyabiashara hao.
Makalla ametoa maagizo hayo leo Alhamisi, Septemba 9, 2021, alipokwenda kusikiliza malalamiko yaliyopo kati ya wafanyabiashara wa maduka na wamachinga katika eneo la Msimbazi Kariakoo.
Amesema kwa kutokana na hali aliyoishuhudia tangu kateuliwa kuwa Mkuu wa mkoa huo, hali aliyojionea alipofika Karikoo leo ni wazi kwamba wanatakiwa wapishe kwanza maeneo ya waenda kwa miguu ambao kwa muda mrefu wamewakosesha haki yao ya kutumia barabara na kusababisha ajali.
Katika maagizo hayo ametoa wiki moja kwa wakuu wa Wilaya wa Mkoa huo kila mtu kwenye eneo lake kukutana na viongozi wa wamachinga kuweka utaratibu wapi watawapelekea wafabiashara hao ili waendelee na shughuli zao za kutafuta riziki.
Pia, ametumia fursa hiyo kuwaeleza wamachinga kwamba serikali inawapenda naa kuwathamini na ndio maana kwenye mikutano mbalimbali hata ya wafanyabiashara wakubwa wamekuwa wakialikwa.
Aidha ameaema licha ya kuwa wanajua wazi kwamba wafanyabiashara hao hawapaswi kuwa maenei hayo lakini hawajataka kutumia nguvu kuaondoa na badala yake kutafuta utaratibuzuri wa kuwapanga.