×

Dk Manyaunyau Aibuka, Akanusha Madai ya Kufungwa

1 2 3 IMG_0515

Picha zikimuonyesha Dk. Manyaunyau akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na  sakata lake hilo.

Jongo Salim ‘Manyaunyau’ ameibuka na kupinga vikali kuwa hajafungwa gerezani kama watu wengi walivyokuwa wanadhani bali kuna mtu mmoja aliyekuwa akitumia jina lake na kuwalaghai watu wengi ambapo mtu huyo aliposomewa mashitaka na kuhumiwa watu walijua ni yeye.

Akizungumza na waandishi wa habari Mlimani City jijini Dar leo, Manyaunyau alisema anawaomba Watanzania wasiingiwe hofu yeye yupo uru bali kuna mtu ayelikuwa akitaka kumchafulia jina.

“ Yaani hii kitu imeniharibia sana jamani,  maana kila mtu anaamini kuwa mimi ndiye niliyefungwa, kitu ambacho si sahihi.  Mimi  bado naendelea na kazi yangu Tabata- Mawenzi mtu yoyote anaweza kuja kuhakikisha hilo,” alisema Manyaunyau.

NA IMELDA MTEMA/GPL

Leave a Comment