
Kiungo wa kati wa Klabu ya Manchester United na Timu ya Taifa ya Ufaransa, Paul Pogba aliisaidia klabu yake kuilaza Newcastle 4-1siku ya Jumamosi kabla ya kujiunga na nyota wa muziki wa Nigeria, Burna Boy kutumbuiza kwa mashabiki.

Pogba ambaye familia yake inatoka nchini Guinea, alicheza pamoja na Cristiano Ronaldo katika uwanja wa Old Trafford huku nyota huyo wa Ureno akifunga magoli mawili baada ya kurejea katika timu hiyo kutoka Juventus.

Mchezaji huyo ambaye ni mshindi mara mbili wa kombe la dunia na Ufaransa, alitoa pasi mbili za magoli na baada ya game hiyo kumalizika alikwenda katika tamasha la muziki la Parklife Music Festival mjini Manchester na kushiriki pamoja na Burna Boy, ambaye alikuwa amevalia tisheti ya Manchester United.
