Rais mpya wa Zambia Mh Haikainde Hichilema , ameelekea Marekani kwenye Mkutano wa UN kwa kutumia usafiri wa watu wote wa ndege ya Qatar Airways , na taarifa zinaonyesha kwamba amepanda daraja la chini kabisa maarufu huko Tanzania kwa jina la (Kajamba nani).
Msafara huo mzito wa Mh Hichilema umeamua kupunguza gharama za safari kwa kuacha ndege binafsi ya Rais ili pesa itakayookolewa ijenge upya Nchi yao kwa lengo la kupunguza Umasikini. Rais Hichilema ameongozana na maofisa wengine Watatu (3) tu .
…………………………………..
Ndugu zangu, tumeondoka nchini tunakwenda kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika New York Marekani, tunaamini mambo mengi mazuri yatajadiliwa kuhusu Zambia na watu wake.
Eneo letu kubwa litakuwa ni sekta ya uchumi, ajira, fursa za biashara, elimu na huduma nzuri za afya kwa watu wa Zambia.
Kama nilivyoahidi wakati naingia madarakani, tutahakikisha rasilimali za Taifa letu zinatumika kwa kwa usawa na zinatunzwa. Hivyo nimeondoka na timu ya watu watatu, Waziri wa mambo ya Nje Stanley Kakubo na na Waziri wa Fedha, Dr Situmbeko Musokotwane.
Mungu awabariki nyote, Mungu aibariki nchi yetu
Hakainde Hichilema
Rais wa Jamhuri ya Zambia
