Naibu waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi, Eng. Stella Manyanya.
Gabriel Ng’osha
MMOJA wa manaibu waziri waliochaguliwa na Rais Joseph Pombe Magufuli, Mhandisi Stella Manyanya aliacha gumzo katika hafla ya kuapishwa kwa mawaziri na manaibu wake baada ya kuanza kujing’atang’ata mbele ya rais.
Gumzo hilo lilitokea wiki iliyopita, siku ya Jumamosi wakati Rais John Pombe Magufuli akiwaapisha mawaziri na manaibu waziri hao katika Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam.
Akijibu gumzo hilo Mhandisi Manyanya alisema; “Siku hiyo nikiwa njiani miwani yangu ilivunjika kioo kimoja kwa hiyo nilijitahidi kusoma bila miwani ndiyo maana nilikuwa napata shida, ingawa kazi kweli ipo na mimi niko tayari kukabiliana nayo.”