×

Gomes Aanza na Kibu, Kanoute Simba

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amefunguka na kuelezea jinsi anavyovutiwa na wachezaji wake wapya, mzawa Kibu Denis na Sadio Kanoute raia wa Mali.

 

Kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa, Gomes aliwaanzisha wachezaji hao kikosi cha kwanza dhidi ya TP Mazembe ambapo Simba walifungwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mkapa mkoani Dar.

 

Akizungumzia viwango vya wachezaji hao, Gomes alisema kuwa: “Ingawa TP wametufunga ila ilikuwa kipimo sahihi sana kwangu kuona kiwango na ubora wa wachezaji wangu kwa kiwango kizuri walichokionyesha hasa kwenye ufundi na namna walivyokuwa wanatengeneza nafasi.

 

“Nimependa sana viwango vya Kanoute na Kibu Denis wameanza vizuri na naimani wakizidi kuzoeana mtaona mengi mazuri kutoka kwao.”

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam

Leave a Comment