
Shabiki wa Simba, MC Mishepu amefunguka kuweka nyumba yake yenye thamani ya Tsh. Milioni 300 endapo Simba akifungwa na Yanga kwenye mchezo wa ngao ya jamii siku ya Septemba 25.
MC Mishepu ambaye anakaa Kijitonyama, Dar es Salaam anasema amefanya hivyo kwa sababu aamini Yanga hawezi kumfunga Simba na ikitokea hivyo wamfuate atatoa hati za nyumba na kuwakabidhi mashabiki wa Yanga.