×

Kifo cha Mohamed Chaacha Majonzi kwa Mke, Mama, Watoto – Video

Kifo cha Mohamed Ramadhan Mkongo, mfanyabiashara ndogondogo au maarufu kama machinga kilichotokea alfajiri ya Septemba 23, 2021 katika eneo la Vingunguti Scania jijini Dar es Salaam, kimeacha simanzi kubwa kwa familia yake iliyokuwa ikimtegemea kuendesha maisha akiwemo mkewe, watoto, mama yake mzazi pamoja na ndugu wengine.

 

Maisha ya Ramadhan yalikatishwa ghafla baada ya kugongwa na gari ambalo mpaka sasa halijafahamika kwa sababu halikusimama baada ya tukio hilo, wakati akiwa anavuka barabarani katika eneo hilo na kuzusha taharuki kubwa.

 

Waandishi wa Global TV, Richard Bukos na Issa Mnally wamefika nyumbani kwa marehemu, Kiwalani Minazi Mirefu jijini Dar es Salaam na kuzungumza na familia yake ambayo kwa masikitiko makubwa imeelezea jinsi ilivyoumizwa na tukio hilo.

Tazama video kusikiliza walichokisema.

Leave a Comment