
KOCHA Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, ameweka wazi kuwa malengo makubwa ya timu yao msimu huu wa 2021/22 ni kuhakikisha wanashinda ubingwa wa Ligi Kuu Bara kama ilivyokuwa msimu wa 2013/14.
Azam juzi ilikuwa na kibarua kigumu cha mchezo wake wa ufunguzi kwa msimu wa 2021/22 ugenini, walipokaribishwa na Coastal Union, wakicheza Uwanja wa Mkwakwani, Tanga na kutoa sare ya bao 1-1.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Bahati alisema: “Baada ya kuwa na mwanzo mzuri katika Kombe la Shirikisho Afrika ambapo timu yetu imefanikiwa kufuzu hatua ya kwanza, sasa ni muda wa kurejea kwenye mashindano mengine muhimu ambayo ni Ligi Kuu Bara.
“Tumekuwa na maandalizi mazuri ya kabla ya msimu, pia tumefanya usajili bora kwa msimu huu wa 2021/22, malengo yetu makubwa ni kushinda ubingwa wa Ligi Kuu, kwa ubora wa kikosi chetu tunaamini hilo linawezekana.”
JOEL THOMAS, DAR